Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Kampeni ya Kitengo cha Wanawake “Ramadhan… Ruwaza ya Kweli ya Mabadiliko”

Mwezi mtukufu wa Ramadhan unatukumbusha kwamba Uislamu ulikuja tu kubadilisha ulimwengu na kutatua matatizo ya wanadamu kulingana na muongozo wa Mwenyezi Mungu (swt) na kwa ruwaza iliyowasilishwa katika Quran na Sunnah. Tunaposhuhudia dhulma, ukandamizaji, na misiba mingi na matatizo yanayoukumba ulimwengu wa Kiislamu na wanadamu kwa jumla, ni wazi kabisa kwamba tunahitaji sana ruwaza sahihi ya mabadiliko iliyo wasilishwa na Uislamu.

Dola, vyombo vya kilimwengu, na mashirika ya kimataifa yamethibitisha kutokuwa na uwezo wao wa kutoa suluhisho bora, endelevu, na lenye mafanikio kwa matatizo ya mataifa au kukomesha mauaji ya halaiki, uvamizi, na mateso ya watu wengi.

Kwa hivyo, mwezi mtukufu wa Ramadhan unapaswa kuwa fursa kwetu kuelewa na kutafakari ruwaza ya kweli ya mabadiliko ya wanadamu kama ilivyowasilishwa katika Quran na Sunna, jinsi ya kuifikia, na dori yetu kama Waislamu katika kufikia lengo hili.

Wakati wa mwezi huu mtukufu, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kitazungumzia maudhui hii, ikiwa ni pamoja na sifa na mabadiliko yanayohitajika kwetu kama Waislamu, kama Umma wa Kiislamu, katika vyama vyetu vya kisiasa, majeshi yetu, na katika ngazi ya dola, ili kufikia ruwaza hii ya kweli ya mabadiliko, pamoja na vikwazo vinavyozuia kuifikia na jinsi ya kuvishinda.

﴿شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْءَانُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَان

“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi.” [Al-Baqara: 185]

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut  Tahrir

Jumatano, 01 Ramadhan 1447 sawia na 18 Februari 2026 M

- Video za Ualishi wa Kampeni ya Ramadhan -

KIINGEREZA:

- Bronschure  ya Kampeni ya Ramadhan -

(Bronchure Hivi Punde)

- Alama Ishara za Kampeni za Ramadhan -

#رؤية_حقيقية_للتغيير

#TrueVision4Change

­- Ili Kufuatilia Kampeni ya Ramadhan Kupitia Mitandao ya Kijamii -

الفيسبوك: QANITATHT1

https://www.facebook.com/QanitatHT1

تويتر: @ALQANITAT

https://x.com/alqanitat

الانستغرام: @WOMEN_SHARIA

https://www.instagram.com/women_sharia?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.