Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  15 Ramadan 1447 Na: 1447 / 15
M.  Jumatano, 04 Machi 2026

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Ustadh Ibrahim Ismail Arar (Abu Khalil)
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]

(Imetafsiriwa)

Kwa imani katika qadhaa ya Mwenyezi Mungu na kukubali mapenzi Yake, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inaomboleza mmoja wa wanachama wake, mbebaji da’wah ya Uislamu:

Ustadh Ibrahim Ismail Arar (Abu Khalil)

Alifariki mnamo Jumanne, tarehe 14 Ramadhan, 1447 H, sawia na 3 Machi 2026 M, akiwa na umri wa takriban miaka tisiini.

Abu Khalil alijiunga na safu ya Hizb katika miaka ya 1960 pamoja na kizazi chake cha kwanza. Alikuwa mchangamfu katika kueneza ujumbe, akisema waziwazi katika kutetea haki, mkarimu, na kujitolea kwa ajili ya lengo na watetezi wake, akijitolea kufanya kazi kuelekea kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amsamehe, amrehemu, na amfanye miongoni mwa wale walioachiliwa huru kutokana na Moto katika mwezi huu mtukufu, na amkusanye pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, na wema katika pepo za juu kabisa na ni maswahaba bora walioje hao! Mwenyezi Mungu awape familia yake na wapendwa wake thawabu kubwa na awatie moyo wa uvumilivu na faraja.

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Kalima ya Sheikh Said Ridhwan (Abu Imad)

katika Kikao cha Kutoa Rambirambi kwa Ustadh Ibrahim Ismail Arar (Abu Khalil), Mwenyezi Mungu amrehemu,

Jumatano, 15 Ramadhani 1447 H - 4 Machi 2026

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.