Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
| H. 4 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H.T.L 1447 / 25 |
| M. Alhamisi, 21 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Msamaha Jumla
Uadilifu Nusu ni Dhulma, na Hakuwezi Kuwa na Msamaha Jumla wa Kibaguzi!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Mei 19, 2026, tovuti ya Lebanon Debate ilichapisha kile ilichokiita toleo la mwisho lililorekebishwa la sheria ya msamaha wa jumla. Ilionekana wazi kwamba sheria hii haikuwa ya jumla, ikiwajumuisha raia wote, bali iliundwa kwa vipimo vya kimadhehebu, ubaguzi, na hesabu finyu, zisizo na uwazi. Inaonyesha mwendelezo wa enzi ya dhulma iliyowekwa na utawala wa Assad mhalifu na wafuasi wake nchini Lebanon, na mtazamo unaokataa kuhama kutoka wazo la udhalimu hadi wazo la haki na usawa. Zaidi ya hayo, ukiukwaji wa kisheria uliibuka katika kuingiliwa kwa kimabavu wakati wa uandishi wa sheria ya msamaha wa jumla! Ni chini ya kanuni gani za kisheria au mifumo ya kimataifa ambapo kitu kama hicho kipo?! Ni katika chombo hiki dhaifu tu, ambacho kinathibitisha kila siku kwamba ni mkusanyiko tu wa madhehebu ambayo nchi imeundwa, si nchi ya kawaida ambapo madhehebu huishi pamoja kama mataifa mengine, mradi tu yachague mfumo wa utawala unaoegemea msingi wa utunzaji wa haki wa raia wake, usio na ukandamizaji na unyanyasaji wa kiholela!
Mtu yeyote anayeifahamu Lebanon anajua kwamba mamlaka tawala huko huyapa kipaumbele maslahi ya waungaji mkono wao wa Magharibi, hasa Marekani, kuliko maslahi ya watu. Hivi ndivyo ilivyo kwa tawala zote zinazotawala katika eneo hilo. Tuna uhakika kwamba mchakato wa uchaguzi na mazungumzo na umbile la Kiyahudi ndivyo vilivyowafanya mamlaka kuleta suala la msamaha wa jumla mbele, wakitarajia kuwavuruga Waislamu na kuwanyamazisha wasitumie ufahamu wao na haki yao halali ya kukataa vitendo na makubaliano yaliyofanywa na utawala wa sasa katika mazungumzo na Wazayuni.
Kuhusu faili la msamaha, tunasema:
Kwa wawakilishi wa Waislamu: Msimamo wenu lazima uwe wa ujasiri zaidi, wazi zaidi, imara zaidi, na karibu zaidi na watu mnaopaswa kuwawakilisha. Mmeona kile ambacho mtaa wa Kiislamu unataka. Msiwe wawakilishi wa mamlaka katika dhulma zao, bali muwe wawakilishi wa watu katika kuondoa dhulma kutoka kwao. Iwapo mutalazimika kuakhirisha sheria hii, basi ima mutoe msamaha wa jumla wa kina ambao unaregesha mambo kwa utaratibu wake ufaao, au mukatae sheria iliyolazimishwa na uhalisia na unyanyasaji wa mamlaka.
[فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيراً]
“Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda.” [An-Nisa:135].
Kwa masheikh wa Waislamu na taasisi zao, hususan Dar al-Ifta na washirika wake: Huu ni wakati wa watu kujua kama nyinyi kweli ni miongoni mwao, au mumejitenga nao kwa kuegemea upande wa mamlaka ya ukweli na maafikiano ya dhulma ya kila aina. Msirekodi msimamo huu dhidi yenu, na kuweni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ]
“Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu” [An-Nisa:135].
Kwa Spika wa Bunge na wale anaowawakilisha, afisi yako ya vyombo vya habari imesema kwamba “unafanya juhudi za kuifikisha nchi kwenye mshikamano na makubaliano ambayo inayahitaji sana leo.” Lakini je, mshikamano na makubaliano yanapatikana kwa kuruhusu kuregea kwa vibaraka wa umbile la Kiyahudi, kuwaachilia huru walanguzi wa dawa za kulevya, na kisha kutengeneza takwimu za kuwaweka wale waliobaki gerezani—yaani, Waislamu ambao ndio wamiliki halali wa sheria hii?! Je, hivi ndivyo mshikamano na makubaliano yanavyoonekana?! Au ni kuhusu kugeuza ukurasa wa yaliyopita—kama baadhi wanavyopenda kuyaita—kwa kuwaondoa gerezani wale waliodhulumiwa na utawala wa Assad na wasaidizi wake nchini Lebanon, hasa baada ya mateso yao na dhulma ya utawala huo wa kihalifu na washirika wake kuthibitishwa?!
[وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ]
“Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” [Al-Ma'idah:8].
Na Waziri Mkuu, hakimu wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki! Je, hii ni haki! Unawezaje kukubali udhalimu huu katika sheria?! Na vipi kuhusu kile Waziri wenu wa Ulinzi alifanya na kile yeye na maafisa wake waliohudhuria kamati walichotangaza?! Kulingana na mfumo wa serikali wa Lebanon, nyinyi ni vyombo vya utendaji vilivyo chini ya sheria, kwa hivyo moja ya taasisi zenu kubwa zaidi inawezaje kuingilia kati waziwazi, na kusababisha rasimu ya sheria ambayo si msamaha wa jumla bali ni maalum?! Hamkupaswa kukaa kimya kuhusu makosa haya na kuendelea kwa dhulma, hasa kwa vile mnatakiwa kuwakilisha upande uliodhulumiwa zaidi nchini. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ إِنَّ اللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ إِنَّ اللَّهَ كَانَ سَمِيعاً بَصِيراً]
“Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” [An-Nisa:58].
Kwa afisi ya rais na enzi mpya, kama mulivyoiita, baadhi walikuwa na matumaini kwamba umechukua madaraka. Katika hotuba yako ya uzinduzi, ulisema: “Haki ndiyo msuluhishi na ulinzi pekee kwa kila raia. Hii ni ahadi yangu! Ahadi yangu ni kufanya kazi nao wote kutetea maslahi ya umma na haki za Walebanoni wote, mmoja mmoja na kwa pamoja. Hakuna dhehebu lililo bora kuliko jengine, na hakuna raia aliye na faida kuliko mwengine. Hii ni ahadi ya kuheshimu katiba, kujenga serikali, na kutekeleza sheria. Hii ni ahadi ya Lebanon!”
Je, unaona kweli ulichoahidi kinachowakilishwa na sheria hii yenye dosari? Je, unaona kweli ndani yake maslahi ya umma ya nchi na watu wake, naam, idadi kubwa ya watu wake? Tunatoa wito kwako ushikamane na kile ulichoahidi katika hotuba hiyo hiyo: “Ahadi yangu ni kupambana na uhalali wa kikatiba wa sheria yoyote inayokiuka vifungu vya katiba na kuheshimu ugavi wa mamlaka, kutekeleza jukumu langu la usimamizi kwa uadilifu na usawa, na kupitia haki yangu ya kukataa sheria na amri ambazo hazitumikii maslahi ya umma, na kuachia Bunge au Baraza la Mawaziri kuzifikiria upya.” Je, utachukua hatua ipasavyo? Je, utashikamana na maneno haya?
Na sasa kwa familia zetu, familia za waliowekwa kizuizini na kufungwa bila haki: Ushindi ni wakati wa subira tu, na mumevumilia na kuvumilia kwa miaka mingi mirefu. Kwa hivyo msikate tamaa, wala msirudi nyuma. Tumewalingania mara kwa mara, na tunarudia wito wetu: Maandamano yenu ya amani mabarabarani yanazingatiwa na mamlaka, na harakati zenu za amani huwasumbua na kuwaogopesha. Kwa hivyo msikae kimya, wala msidharau harakati zenu. Lakini jihadharini, jihadharini msivutwe katika kishawishi cha kukabiliana na taasisi zenye mamlaka, hasa wanajeshi na vikosi vya usalama. Tatizo letu si lao, bali la wale waliokubali kutengwa kwa wana wetu kutoka kwa msamaha wa jumla, na kuugeuza kuwa msamaha maalum, ambao lazima tuukatae kabisa. Kuachiliwa huru kwa wana wetu sio fadhila, bali ni haki halali, isiyo na mzozo au mjadala. Hakika, ni jambo dogo sana wanalostahili baada ya miaka mingi ya dhulma na mateso kwa ajili yao na kwa ajili yenu. Tunawakumbusha maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ]
“Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa.” [Aali 'Imran 3:200].
Kwa kutamatisha, kwa wanasiasa wa Lebanon: Dhulma ina matokeo mabaya sana, Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَمَنْ يَظْلِمْ مِنْكُمْ نُذِقْهُ عَذَاباً كَبِيراً]
“Na atakaye dhulumu miongoni mwenu tutamwonjesha adhabu kubwa.” [Al-Furqan 25:19]. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَالظَّالِمُونَ مَا لَهُمْ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ]
“Na wenye kudhulumu hawana mlinzi wala msaidizi.” [Ash-Shuraa 42:8]. Mtume (saw) amesema: «اتَّقوا الظلم؛ فإنَّ الظلم ظلماتٌ يوم القيامة» “Iogopeni dhulma, kwani hakika dhulma ni magiza Siku ya Kiyama.” Na Mwenyezi Mungu Mtukufu asema katika Hadith Qudsi: «يَا عِبَادِي، إِنِّي حَرَّمْتُ الظُّلْمَ عَلَى نَفْسِي وَجَعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّماً، فَلَا تَظَالَمُوا» “Enyi waja wangu, hakika Mimi nimeharamisha dhulma juu ya nafsi yangu na nikaijaalia kuwa haramu baina yenu, basi msidhulumiane.” Hivyo ogopeni, ogopeni dhulma na matokeo yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «إِنَّ اللَّه لَيُمْلِي لِلظَّالِمِ فَإِذَا أَخَذَهُ لَمْ يُفْلِتْهُ» “Hakika, Mwenyezi Mungu humpa muda mwenye kudhulumu, lakini pindi anapomkamata hamruhusu kutoroka.” Kisha yeye (saw) akasoma:
[وَكَذَلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَى وَهِيَ ظَالِمَةٌ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ]
“Na ndio kama hivyo ndivyo inavyo kuwa Mola wako Mlezi anapo ikamata miji inapo kuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali.” [Hud 11:102].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |