Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina):

Wanawake Huru wa Palestina Wanawazungumzia wale Wanaowafisidi Wanawake na Kuunga Mkono Makubaliano ya CEDAW!

Umati mkubwa wa wanawake kutoka Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina waliitikia wito wa dada zao huko Khalil (Hebron) kwa mkutano wa kipekee wa kujadili hukmu za Kiislamu kuhusu wanawake na familia za Kiislamu. Lengo lilikuwa kuwalinda na kuwaelimisha dhidi ya kampeni za Magharibi na ufisadi zinazotaka kuwaangamiza, na hivyo, familia na jamii, kupitia mbinu na njia mbalimbali.

Mkutano huo, au tuseme kongamano hilo, lilijumuisha hotuba kadhaa, ya kwanza ikiwa na kichwa "Wanawake Kati ya Hadhi Iliyohifadhiwa na Wahyi na Kaulimbiu Zinazogongana Juu Nao." Hotuba hii ilifafanua hadhi ya wanawake katika Uislamu, jinsi wahyi ulivyohifadhi utukufu, hadhi, na haki zao, na majaribio ya Magharibi na washirika wake kupotosha na kubadilisha hili.

Hotuba ya pili, yenye kichwa "Shambulizi Kali la Magharibi dhidi ya Wanawake," ililenga hukmu za Kiislamu zinazohusiana na mfumo wa kijamii, hasa mchanganyiko wa wanaume na wanawake na kuondolewa kwa vizuizi kati yao.

Hotuba ya tatu, yenye kichwa "Makubaliano ya CEDAW na Matokeo Yake: Vita dhidi ya Hukmu za Kiislamu na Kuwafisidi Wanawake Waislamu," ilionyesha mgongano kati ya vifungu kadhaa vya Mkataba wa CEDAW na hukmu za Kiislamu, ambao unatafuta kuvilazimisha kwa wanawake wa Kiislamu.

Hotuba ya nne, yenye kichwa "Harakati ya Wanawake Nchini Palestina: Mavuno Machungu," ilizungumzia suala la ufadhili wa kigeni na pesa zenye shaka zinazotumiwa na mashirika na vyama vya wanawake vinavyolenga kuwaharibu wanawake na familia.

Hotuba ya tano, yenye kichwa "Kuchanganya Kati ya Wanaume na Wanawake: Miongozo na Hukumu," ilichunguza dhana ya mchanganyiko kati ya jinsia kutoka kwa mtazamo wa kisheria wa Kiislamu, ikielezea miongozo na hukmu zinazosimamia uhusiano kati ya wanaume na wanawake katika maisha ya faragha na ya umma, na pia kwenye mitandao ya kijamii.

Hotuba ya sita, yenye kichwa "Uwezeshaji wa Wanawake," ilionyesha hatari ya kauli mbiu hii, ambayo imeenea katika mazungumzo ya kisasa kuhusu wanawake, na hatari ya athari yake na matokeo yake kwa mbinu za udanganyifu.

Kufuatia hili, ujumbe uliorekodiwa kutoka kwa dada mmoja kutoka Gaza Hashim uliwasilishwa kwa mashirika ya wanawake, ukizungumzia dori yao katika mateso ya wanawake mjini Gaza, ikiwa ni pamoja na mauaji, uhamisho, hasara, shida, mateso, na kufungwa.

Hotuba ya kumalizia ilikuwa ujumbe wazi kutoka kwa wanawake wa Khalil (Hebron), wakitangaza kukataa kwao ajenda za Magharibi, Mkataba wa CEDAW na makubaliano yake husika, na chochote kinachogongana na sheria ya Kiislamu na hukmu zake.

Na kwamba Palestina ilikuwa na inabaki kuwa Ardhi Iliyobarikiwa ambayo wanawake na wanawake huru watabaki kuwa ngome isiyoweza kushindikana dhidi ya majaribio yote ya Umagharibi na ufisadi.

Shairi lilisomwa, lenye kichwa "Ewe Lulu, Ulihifadhiwa Jana kwa Thamani Kubwa."

Mkutano au kongamano lilijumuisha onyesho la video mbili. Video moja ilionyesha vipengee vya giza vya uhalisia wa wanawake katika jamii za Magharibi, ambavyo wanataka wanawake wa Kiislamu waige.

Video ya pili ilizungumzia baadhi ya mipango na mawazo yaliyopangwa dhidi ya wanawake wa Kiislamu.

Kongamano lilimalizika kwa dua ya kusisimua ya uthabiti, tamkini, na ulinzi wa wanawake na mabinti wa Kiislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na kila mahali.

Jumamosi, 7 Rabi' al-Thani 1448 H, sawia na 19 Septemba 2026 M

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

- Sehemu ya Shughuli ya Amali -

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina):

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Chaneli ya YouTube Wito kutoka Bait al-Maqdis

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.