Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Trump Mtawala wa Kiimla na Mtoto wake, Umbile la Kizayuni, Wameanzisha Shambulizi la Kikatili dhidi ya Iran

(Imetafsiriwa)

Amerika na umbile la Kiyahudi walizindua shambulizi kubwa la pamoja dhidi ya Iran siku ya Jumamosi, huku milipuko ikitikisa mji mkuu, Tehran, na miji mingine kadhaa, ikiwemo Qom, Isfahan, Kermanshah, na Karaj. “Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuanza kwa shambulizi dhidi ya Iran, akisema, “Tumeanza tu operesheni kubwa za mapigano nchini Iran.” Channel 12 ya ‘Israel’ iliripoti kwamba “Israel” ilishambulia shabaha kadhaa za serikali ya Iran.” (Al Jazeera, 28/2/2026). Trump aliendelea na kauli zake za kiburi, akidai kwamba Amerika na jeshi lake ndio walio imara na wenye nguvu zaidi duniani na kwamba hangeiruhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia na makombora. Mtoto wake, Netanyahu, aliunga mkono kauli za Trump. Iran, kwa upande wake: “Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi alisema kwamba nchi yake itatumia uwezo wake wa kijeshi kujilinda ndani ya mfumo wa haki yake ya asili ya kujilinda halali.” (Al Jazeera, 28/2/2026). Iran ilirusha makombora dhidi ya umbile la Kiyahudi na katika kambi za Marekani katika Ghuba.

Kwa hivyo, ndege za kivita za umbile la Kiyahudi na ndege za Marekani, kutoka nchi kavu, baharini, na angani, zilizindua shambulizi leo kwenye kambi za kijeshi na vituo vya serikali nchini Iran, zaidi zikiwa zimejikita katika mji mkuu, kwenye makao makuu ya serikali, na kwenye makao makuu ya Kiongozi Mkuu na Rais. Taarifa zao za awali zilionyesha kuwa mashambulizi haya yangedumu kwa siku nne hadi kumi na yanaweza kuwa wazi hadi programu za nyuklia na makombora za Iran zitakapovunjwa. “Duru za Israeli zilionyesha kuwa awamu ya kwanza ya mashambulizi inaweza kudumu kwa siku nne, ikizingatiwa kuwa ni mwendelezo wa vita vya siku 12 vilivyozinduliwa msimu uliopita wa kiangazi mnamo Julai 2025. Wakati huo huo, duru moja ya Marekani ilisema kwamba kampeni ya sasa ya kijeshi ya Marekani inaweza kudumu kwa takriban siku 10, kulingana na CBS News.” (Al-Arabiya, 28/2/2026)

Enyi Waislamu:

Shambulizi hili la kikatili linafanywa dhidi ya Iran wakati ambapo ilikuwa ikizunguka katika duara la ushawishi la Amerika, ikiipa huduma katika vita vyake dhidi ya Iraq, Afghanistan, na sehemu nyingine nyingi za eneo hilo. Amerika haikuzungumzia suala la makombora na silaha za nyuklia na Iran. Kwa kweli, Obama alihitimisha makubaliano ya 2015, pamoja na ushiriki wa nchi za Ulaya, na kuruhusu Iran kurutubisha urani hadi 3.67%. Iran ilibaki ndani ya mzunguko wa Amerika wakati wa miaka hiyo, kama vile Uturuki. Kisha, wakati mtawala Trump alipoingia madarakani, alitaka Iran iwe nchi yake kibaraka, inayomtii, inayosema anachosema na kufanya anachotaka. Hapo awali iliingia katika mazungumzo ya udanganyifu jijini Muscat, ambayo yalidumu kwa takriban raundi tano. Kisha yakaja mashambulizi ya Trump na Mayahudi, yaliyopewa jina la “Vita vya Siku 12,” ambayo ndiyo hasa yaliyotokea. Trump alitangaza kulenga vituo vitatu vya nyuklia vya Iran, akithibitisha mafanikio ya shambulizi la Marekani. Alionyesha kwamba maeneo ya nyuklia ya Fordow, Natanz, na Isfahan yalilengwa, akiitaka Iran kufanya amani na kukomesha vita. Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alithibitisha kwamba shambulio la Marekani lilikuwa limeondoa matarajio ya nyuklia ya Iran. (BBC, 22/6/2025).

Mashambulizi hayo hayakufanikiwa kuifanya Iran ihame kutoka nchi inayozunguka katika mzunguko hadi nchi kibaraka. Badala yake, inaonekana sauti zilionekana, ingawa ni chache, zikitaka kujitenga hata kutoka kwenye mzunguko huo. Kwa hivyo, Amerika ilirudi kwenye ujanja wa mazungumzo tena, ikizingatia masuala yale yale, yaani kupokonya silaha za makombora na nyuklia za Iran. Na kama ilivyotokea katika raundi ya kwanza na shambulizi baada ya raundi tano, ilitokea sasa na shambulizi baada ya raundi tatu!

Enyi Waislamu:

Watawala katika nchi za Waislamu wameshindwa kuelewa uzito wa kuwa washirika wa makafiri, na kwamba huleta fedheha katika ulimwengu huu na adhabu kali Akhera.

[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِنْدَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعاً]

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [An-Nisa: 139].

Hawatambui kwamba mataifa ya makafiri kimsingi yanajishughulisha na maslahi yao wenyewe na yana chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu mchana na usiku. Ikiwa wataonyesha kuridhika na nchi inayozunguka katika duara lao la ushawishi au hata pamoja na vibaraka wao, ni kwa sababu hawawatakii mema, bali wanaficha na kutangaza uovu. Ikiwa watawala hawa, iwe wanazunguka katika duara lao la ushawishi au ni vibaraka wao, wataelewa kwamba Amerika haiwathamini ikiwa maslahi yake yanahitaji waondolewe, wangejifunza kutokana na mafunzo ya historia. Je, ni vibaraka wangapi ambao Amerika imewatupilia mbali baada ya kumaliza dori yao ya kuwatumikia? Kama watawala hawa wangekuwa na akili yoyote, wangewakataa makafiri mithili ya mbegu, lakini ni viziwi, mabubu, na vipofu, na hawatarudi. Utiifu wao kwa wakoloni makafiri umefikia hatua ambapo pindi nchi zao zozote zinaposhambuliwa, zengine hazisongi kuzisaidia. Bora wanachofanya ni kuhesabu maiti na majeruhi! Kama ilivyo hali katika shambulizi dhidi ya Iran.

Enyi Waislamu:

Izza yenu iko katika kurudi kwa Khilafah Rashida yenu. Kiongozi, Hizb ut Tahrir, asiyewadanganya watu wake, imejitolea kwa kazi ya dhati na nzito, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ili kuregesha mfumo kamli wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida. Kwa kweli ni chama kiongozi kisicho wadanganya watu wake, chama ambacho kheri yake inang’aa, na ambacho wote ambao hawawezi kuvumilia kheri yake hujitenga nacho. Hivi ndivyo tunavyokiona, na tunaamini wanachama wake wote wanaofanya kazi nacho ni wafanyikazi makini, wenye bidii, na waaminifu, wanaotamani, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Akhera kuliko yote, hata zaidi kuliko ulimwengu huu. Wanajitahidi mchana na usiku, wakitarajia rehema ya Mwenyezi Mungu, kwamba ahadi Yake na bishara njema za Mtume Wake (saw) ziweze kutimizwa kupitia wao. Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu kulitimiza.

Hili ndilo litakalookoa Ummah, kuregesha izza yake, kuimarisha nguvu zake, na kuwafanya maadui zake wafikiri mara elfu kabla ya kuushambulia. Hii ni kwa kurudi kwa Khilafah yake na dunia kung'aa kwa kheri na uadilifu wake. Kama vile Khilafah ilivyomaliza kiburi cha Kaisari na Kisra na watu wao, ndivyo pia itamaliza kiburi cha wafuasi wao, kama vile Trump mtawala na wenzake miongoni mwa wakoloni makafiri.

Ama kwa umbile la Kiyahudi, ni duni sana kuweza kupewa uzito wowote, kwani ni kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:

[لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

“Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.” [Aal-i-Imran: 111].

Halina uwezo wa kusimama kidete lenyewe; Haliwezi kupigana ila kwa msaada wa watu, kama anavyosema Al-Qawi Al-Aziz:

[ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ]

“Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu.” [Aal-i-Imran: 112].

Wameikata kamba ya Mwenyezi Mungu, wakibakia tu na kamba ya watu—Marekani, Ulaya, na vibaraka wao, watawala wasaliti katika nchi za Waislamu—ambao wamebakia kutoguswa na uvamizi wa kikatili wa Mayahudi. Tatizo liko katika dola zilizopo katika nchi za Waislamu leo, kwani watawala wao wanashirikiana na wakoloni makafiri, maadui wa Uislamu na Waislamu. Hivyo, msiba wa Waislamu uko katika watawala wao na utiifu wao kwa wakoloni makafiri. Wanatii amri zao na kujiepusha na yale wanayokataza, badala ya utiifu wao kuwa kwa Mwenyezi Mungu (swt), kushikamana na sheria Zake, kujitahidi katika njia Yake, na kufuata mfano wa Mtume Wake (saw). Wakifanya hivi, Uislamu na Waislamu wataheshimiwa, na ukafiri na makafiri watadhalilishwa.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

H. 11 Ramadan 1447
M. : Jumamosi, 28 Februari 2026

Hizb-ut-Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.