Hatimaye, Dhalimu Trump Anahitimisha Ziara yake katika Kanda hii
- Imepeperushwa katika Hizb ut-Tahrir
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Trump alianza ziara yake nchini Saudi Arabia mnamo Mei 13, 2025, ikifuatiwa na Qatar mnamo Mei 14, 2025, akihitimisha safari yake nchini Imarati mnamo Mei 15, 2025, na kuhitimisha ziara yake mnamo Mei 16, 2025. Kisha aliandamanisha ziara hii kwa udanganyifu wake kwamba hatazuru umbile la Kiyahudi, kuwakejeli wajinga wanaodai kuwa uungaji mkono wa Trump kwa umbile la Kiyahudi umetikiswa! Hii ni licha ya ukweli kwamba umbile la Kiyahudi lilipanua mashambulizi yake kwenye Ukanda wa Gaza baada ya Trump kuondoka katika nchi hizo tatu.