Ijumaa, 03 Ramadan 1447 | 2026/02/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Sha'aban 1447 Na: H 1447 / 050
M.  Jumanne, 17 Februari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tangazo la Matokeo ya Kuutafuta Mwezi Mwandamo wa Ramadhan Iliyobarikiwa ya Mwaka 1447 H

(Imetafsiriwa)

 Bismillahi Ar-Rahman Ar-Rahim, rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, maswahaba zake, na wale wanaomuunga mkono,

Al-Bukhari amepokea katika Sahih yake kupitia kwa Muhammad ibn Ziyad, aliyesema: Nilimsikia Abu Hurayrah (ra) akisema: Mtume (saw) amesema, au alisema: Abu al-Qasim, rehma na amani zimshukie pamoja na jamaa zake, alisema: «صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ، فَإِنْ غُبِّيَ عَلَيْكُمْ فَأَكْمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلَاثِينَ» “Fungeni kwa kuonekana kwake, na fungueni kwa kuonekana kwake; na ikiwa mutazibwa na mawingu (musiuone), basi kamilisheni Sha’aban siku thalathini.”

Kutokana na hayo, na baada ya kuchunguza mwezi mpya wa mwezi mtukufu wa Ramadhan usiku huu, mkesha wa kuamkia Jumatano, kuonekana kwa mwezi mpya kumethibitishwa kama muonekano halali kwa Kisharia, na hilo ni katika baadhi ya nchi za Waislamu. Kwa hivyo, kesho, Jumatano, ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka huu wa 1447 H.

Kwa mnasaba huu, nawasilisha pongezi zangu, na pongezi za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wote wanaofanya kazi humo, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, nikimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampatie nusrah (ushindi), na atupe ushindi na tamkini kutoka kwake, ili tuweze kutoa ahadi ya utiifu (bayah) kwake kama Khalifa wa Waislamu, mapema kuliko baadaye.

Vile vile, Hizb ut Tahrir, pamoja na Amiri wake na Mashababu wake (wanaume na wanawake) kote ulimwenguni, kwa unyenyekevu inamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dua ya dhati kwamba mwezi wa Ramadhan mwaka huu uwe mwezi wa kheri, baraka, na rehema, na kwamba usipite isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu ameupa Ummah wa Kiislamu ushindi na tamkini. Pia tunamwomba Yeye (swt) awashushie utulivu wake wale walioachwa kulala chini, wakiwa wamenyimwa joto na chakula, ili kulipiza kisasi kwa wale waliowasaliti. Hakika, Yeye ndiye Msikiaji wa dua.

Ramadhan inakuja mwaka huu huku Ummah ukisimama kwenye njia panda mpya; kwa upande mmoja unageuka kwenye makaa ya hali ya ukoloni na miiba ya usaliti wa watawala, na kwa upande mwingine hali mpya zinazoibuka za kimataifa, haswa migogoro ya kafiri Magharibi ya kikoloni imetoa fursa mpya ambazo, ikiwa zitakamatwa, zingesababisha Ummah wa Kiislamu kuinuka kwa muda mrefu.

Mfumo wa kisiasa, usalama, na kiuchumi wa Magharibi umefichuliwa katika kukabiliana na migogoro inayoongezeka. Utekaji nyara wa Rais wa Venezuela, uhalifu wa umbile la Kiyahudi katika ardhi za Waislamu, kiburi cha Marekani mpya, na kufichuliwa kwa ukweli wa mashirika ya kimataifa kama zana za ukoloni, ambazo mara tu manufaa yake yalipoisha ziliachwa pamoja na kanuni zake za uongo kwa kufumba na kufumbua—maendeleo haya yote yanafungua milango zaidi mbele ya Umma wa Kiislamu ili kujiondoa kwenye gereza la Sykes-Picot ambalo ukoloni uliliweka juu yake.

Hata hivyo, kile ambacho Umma lazima ujihadhari nacho leo ni kampeni mpya ya udanganyifu na taarifa potofu. Kinyume na makadirio yote ya juu juu yanayojaza skrini za vyombo rasmi vya habari, tishio la kijeshi si tishio kubwa tena kwa Umma wa Kiislamu. Afghanistan, Iraq, Syria, na Gaza zinashuhudia kwamba Umma wa Kiislamu ni imara na hauwezi kupigwa kwa pigo la mwisho hata kama vita vitaendelea dhidi yake. Badala yake, hatari kubwa zaidi kwa Umma wa Kiislamu leo ​​ni bomu la uongo ambalo watawala wasaliti wanajaribu kulitupa kwa rai jumla ya umma na akili za wanafikra na watu wenye ushawishi kutoka miongoni mwa watu wenye ikhlasi wa Umma wa Kiislamu. Watawala wasaliti na ruwaybidha (watawala duni na watepetevu) waliowazunguka, miongoni mwa kalamu za kukodishwa na wengine wanaotapatapa wanajaribu kukuza fikra za kushindwa na kurudi nyuma kupitia falsafa ya fahamu za kusalim amri na uhalalishaji wa watawala wasaliti mbele ya kafiri Magharibi ya kikoloni kwa kisingizio cha werevu na ujanja. Hivyo, tishio la kijeshi sio tishio la msingi tena kwa Umma wa Kiislamu. Badala yake, tishio la msingi ni kwamba Umma unaamini simulizi ya uwongo kwamba ni Umma dhaifu na usio na uwezo, na kwamba wakati haujafika wa kujikukuta kutoka kwenye vumbi la ukoloni.

Ukweli ni kwamba Waislamu wana nguvu ikiwa watafuata uongozi mmoja, wa dhati, na wenye utambuzi; kwani wanamiliki utayari, dhamira, na azimio la kutosha la kulazimisha uhalisia wanaotaka kwa adui yao haraka kuliko uwezo wake wa kukabiliana na uhalisia huo. Tumeona hili likitokea katika miongo iliyopita wakati wowote Umma ulipomshangaza adui yake na kuanzisha hatua ya dhati katika ardhi yake. Laiti, wakati ulipokuwa ukitekeleza mishangao hii, ulimiliki kitu kilichopangilia uwezo wake na kulenga nguvu zake, ungeweza kuvuna matunda yake na kufaidika nayo kwa natija.

Hapa inakuja dori ya Khilafah. Khilafah, kwa Ummah wa Kiislamu, ndiyo mfumo pekee wa kisiasa na kiutawala unaoweza kupanga na kuamsha uwezo wake. Hivyo basi, Waislamu walipokuwa na Khilafah, idadi yao ilikuwa na athari nzuri na walikuwa nguvu ya kukumbukwa. Sifa yao ya kihadhara na kazi za kiraia zilikuwa na matokeo ya kimataifa ambayo yameendelea hadi leo. Katika historia yote ya Waislamu, Dola ya Khilafah, pamoja na Khalifa wake na majeshi yake makubwa, ilikuwa tayari kumkata kichwani mtu yeyote ambaye Shetani alimnong'oneza kwamba Waislamu ni tonge rahisi kwa wenye tamaa. Hakika, miongoni mwa wale wenye tamaa ni wale ambao Khilafah ilifuta uwepo wao, na kusalia tu alama baada ya kuwahi kuonekana.

Ama kuhusu watawala Ruwaybidha walioketi kwenye viti vya enzi vya dola za Sykes-Picot, wakiwa wamevaa barakoa ya ubwana bandia ili kuwadanganya watu wao ili kuwazuia kuungana na watu wengine wa Ummah wa Kiislamu, hii hapa ndio hali yao katika mikao ya kimataifa, mithili ya mtu anayekaa kando ya bwana wake kwenye meza za maamuzi ya kisiasa duniani, akisubiri maagizo yake kuyatekeleza, ambayo mara nyingi ni maamuzi ya kuogofya dhidi ya Waislamu.

Kwa hivyo, katika mwezi huu mtukufu, tunawataka Waislamu wote kuifanya Ramadhan mwaka huu kuwa zaidi ya kuwa mwezi wa kufunga, Qur’an, swala ya usiku, na sadaka pia kuwa mwezi wa kuzingatia, kutafakari, kuona, na kufikiria upya Khilafah, na jinsi ilivyo kwa njia ya Utume na ni faradhi juu yao ambayo hairuhusiwi kuichelewesha. Na kwamba mwezi huu usiishe isipokuwa wameweka mikono yao kwenye mikono ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir, ili Mwenyezi Mungu atujaalie sisi na wao kufaulu kwa ushindi wa karibu, ambao kwa huo tutasimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَحَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَسَى اللَّهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ الَّذِينَ كَفَرُواْ وَاللَّهُ أَشَدُّ بَأْساً وَأَشَدُّ تَنكِيلاً]

Na wahimize Waumini. Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulio ya walio kufuru. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkali zaidi wa kushambulia na Mkali zaidi wa kuadhibu.” [Surat An-Nisa: 84].

Pia tunawaomba wale wanaofanya kazi katika vyombo vya habari, tovuti, na majukwaa miongoni mwa watungaji rai jumla ya umma kufuatilia amali ambazo Hizb ut Tahrir itazifanya katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kote ulimwenguni, na kuchangia kuzieneza na kuzilingania. Tunawakumbusha kwamba wanachama wa Hizb ut Tahrir wamebeba amana ya kujali rai jumla ya umma, kutoa ushauri, na kuongoza hisia za Waislamu na mtazamo wao kuelekea masuala muhimu, na hakuna kadhia muhimu zaidi leo kwa Waislamu kuliko kadhia ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Msikose fursa ya kuchangia katika kutimiza faradhi hii kubwa, kwani Mwenyezi Mungu atatuuliza kuhusu kile Alichotupa amana. Yeye (swt) amesema: [وَقِفُوهُمْ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ] Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa.” [Surat As-Saffat: 24].

Mwezi wenu uwe wenye baraka. Wasalaamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatahu.

Mkesha wa kuamkia Jumatano ndio tarehe moja ya mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan, wa mwaka wa Hijri wa 1447.

Mhandisi Salah Eddin Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizbut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu