Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
| H. 1 Muharram 1448 | Na: H 1448 / 001 |
| M. Jumanne, 16 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Tunisia Itaendelea na Uzembe Wake Hadi Lini na Kuruhusu Malori Haya ya Kifo Kuchukua Maisha ya Wafanyikazi wa Kike wa Mashamba?
(Imetafsiriwa)
Ghadhabu na hasira ziliongezeka nchini Tunisia wiki iliyopita kufuatia ajali nyingine mbaya, wakati huu katika wilaya ya Mazouna katika jimbo la Sidi Bouzid. Ajali hiyo iliwaacha wafanyikazi kadhaa wa kike wa shambani wakiwa wamejeruhiwa na wawili wakiwa wamekufa katika eneo la tukio. Tunisia inashuhudia kujirudia kwa matukio kama hayo kutokana na serikali kushindwa kukomesha usafiri usiodhibitiwa na kuboresha hali mbaya ya wafanyikazi wa kike wa mashamba! Bila shaka, serikali hii inakwepa kutoa tarakimu na takwimu sahihi zinazoonyesha ukubwa wa janga hilo!
Jukwaa la Haki za Kiuchumi na Kijamii la Tunisia lilitangaza mnamo Oktoba 2025 kwamba ajali 91 zinazotokana na usafiri usiodhibitiwa wa wafanyikazi wa kike wa shambani zilikuwa zimerekodiwa tangu 2015, na kusababisha vifo 68 na majeruhi 1029! Pia ilibainisha kuwa 60% ya ajali zote zilitokea baada ya 2019, kufuatia kutungwa kwa sheria inayodhibiti usafiri wa wafanyikazi wa kike na kiume wa shambani, na kwamba 50% ya ajali hizi zilirekodiwa katika majimbo ya Kairouan na Sidi Bouzid!
Kulingana na wataalamu na wajuzi katika uwanja huo, sheria ya 2019 kuhusu usafiri wa wakulima wa kike haijatekelezwa, hata baada ya amri ya serikali kutolewa. Hii ni kwa sababu ilijumuisha taratibu ngumu na kwa sababu serikali iliacha tatizo la usafiri kwa vyombo vya kibinafsi kushughulikia! Janga hili linathibitisha zaidi kufeli kwa sheria na kutochukua hatua kwa serikali katika kuwalinda wafanyikazi wa kike wa shamba waliotengwa, ambao wanaendelea kufanya kazi katika hali hatarishi na ngumu na wanalazimika kusafiri kila siku katika usafiri usio salama na usiodhibitiwa!
Kufuatia sheria ya 2019, Amri Nambari 4 ya 2024, kuhusu mfumo wa ulinzi wa kijamii kwa wafanyikazi wa kike wa shamba, ambayo pia ilitolewa, pia imebaki kuwa utaratibu tu kwenye karatasi na imeshindwa kupunguza mateso yao hata kidogo.
Kujirudia kwa matukio haya ya kusikitisha katika miaka iliyopita hakuwezi tena kuchukuliwa kuwa ajali tu. Kwa kweli, ni matokeo yasiyoepukika ya uzembe wa serikali na ukosefu wa nia ya kweli ya kushughulikia matatizo ya usafiri, ajira, na ulinzi wa kijamii katika maeneo haya yaliyoathiriwa!
Licha ya kilio kufuatia kila ajali, ahadi na hatua rasmi bado hazitoshi kushughulikia ukubwa wa majanga. Ukosefu wa waangalizi madhubuti wa usafiri usiodhibitiwa unaendelea hadi leo, kama vile kushindwa kutoa njia badali za usafiri. Zaidi ya hayo, utumizi mbaya wa wanawake wanaofanya kazi katika maeneo ya vijijini na kunyimwa haki zao unaendelea!
Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu Umar ibn al-Khattab (ra), ambaye alisema, “Kama nyumbu angejikwaa Iraq, Mwenyezi Mungu (swt) angeniuliza kuhusu hilo: ‘Kwa nini hukuitengeneza barabara, Umar?’” Kwa hivyo, vipi kuhusu maisha ya wanadamu yanayopotea kila mara, chini ya macho na masikio ya watawala nchini Tunisia, bila wao kumcha Mwenyezi Mungu (swt) au kutimiza majukumu yao kwa wanawake hawa!
Enyi watawala wa Tunisia: Maisha ya wafanyikazi hawa wa kike wa shambani si idadi tu iliyoongezwa kwenye orodha ya ajali; ni roho zitakazowawajibisha Siku ya Kiyama, wakimlalamikia Mwenyezi Mungu (swt) kwa uzembe wenu, kufeli kwenu, na usaliti wenu! Kama mungemcha Mwenyezi Mungu (swt) kweli, mungefanya kile kinachohitajika na kukomesha misiba hii. Mungejitahidi kuwaokoa wanawake wa vijijini kutokana na umaskini, unyonyaji, kutengwa, na mapambano makali ya maisha duni, ambayo mara nyingi yametiwa madoa ya damu! Kwa hivyo, mcheni Mwenyezi Mungu (swt) katika kile alichokikabidhi kwenu! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللَّهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّته إِلَّا حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ» “Hakuka mja yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atamteua kuwa mtawala juu ya watu, akafa huku akiwa anawadanganya raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu amekwisha mharamishia Pepo.” (Bukhari na Muslim).
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizbut-tahrir.info |



