Jumatatu, 23 Rajab 1447 | 2026/01/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Lazima Tuitupilie Mbali Miungu ya Uongo na Miovu ya Utaifa na Ukabila Kwenye Jaa la Historia!

Kutokana na utaifa, ukabila na kuanzishwa kwa dola za kitaifa na mipaka yake katika ardhi za Waislamu, kitambulisho cha Waislamu kimeharibika na kutengana, ambapo Ummah wa Kiislamu hapo awali uliunganishwa katika udugu mmoja na ndani ya Dola moja ya Kiislamu, badala yake ukagawanyika katika dola za kitaifa zaidi ya 50 na vitambulisho vya kitaifa kufuatia kuvunjwa kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab, 1342, mikononi mwa Mustafa Kamal, “baba wa udhalifu”.

Soma zaidi...

Dori ya Magharibi Kafiri katika Kuuchana Umma wetu na katika Kuivunja Khilafah yetu, Nembo ya Nguvu Yetu

Tulipokuwa Umma mmoja tofauti na mwingine wowote, dola yetu iliweka Rayah (bendera) yake juu ya maeneo yote; ilikuwa mlinzi, kimbilio, na kizuizi dhidi ya yeyote ambaye angeweza hata kufikiria kumshambulia Muislamu mmoja. Waislamu walikuwa mwili mmoja, wakisaidiana kwa ushindi, msaada, na kuimarishana. Iwapo kiungo kimoja kingelalamika, mwili uliobaki ungejibu kwa kukesha na homa. Kisha maadui walielewa kwamba umoja huu na dola hii ndio sababu ya nguvu ya Umma wa Kiislamu na ngao yake ya kinga. Kwa hivyo walianza kulenga ngao hiyo, wakijaribu kuivua, wakifanya juhudi kubwa kwa miaka mingi mirefu hadi walipofikia lengo lao, kwa masikitiko, na kuivunja Dola ya Khilafah mnamo 1924, wakiuchana Ummah wa Uislamu vipande vipande ili kuizuia kurudi katika hali yake ya zamani.

Soma zaidi...

Rajab na Suala la Umoja wa Waislamu

Kwa Waislamu wengi leo, neno “Khilafah” huhisika kama jambo la mbali. Baadhi hulihusisha na vitabu vya historia, wengine huliona kama jambo la kindoto au lisilo la kawaida. Hili linaeleweka, hasa kwa kizazi ambacho kimewahi kuishi ndani ya mfumo wa kisasa wa dola ya kitaifa. Lakini kila mwaka, mwezi wa Rajab hutukumbusha kimya kimya mabadiliko makubwa katika historia ya Waislamu. Katika Rajab 1924, Khilafah ilifutwa. Huu haukuwa tu mwisho wa serikali, bali kupotea kwa muundo uliopangilia umoja wa Ummah wa Kiislamu kwa zaidi ya karne kumi na tatu.

Soma zaidi...

Kuangazia Njia ya Shariah Inayofuatwa na Hizb ut Tahrir Kusimamisha Dola

Uhalisia wa sasa wa Waislamu leo ​​ni sawa na awamu ya Makka ya ujumbe wa Mtume, kwani wanaishi katika “Dar ul-Kufr” (Nyumba ya Ukafiri) kutokana na kutawaliwa na sheria zisizokuwa zile zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) na neno “Dar” ni istilahi ya kifiqhi iliyofafanuliwa kwa kina katika vitabu vya fiqh (Fiqh ya Shariah). Hili linalazimu kufuata njia ya mabadiliko ya Makka. Mtume (saw) alifuata hatua tatu kuu katika njia yake ya kusimamisha dola ya Kiislamu.

Soma zaidi...

Kusimamishwa kwa Khilafah Rashidah na Dori Yetu

Kuna mijadala mingi kuhusu kusimamishwa kwa Khilafah siku hizi katika Ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi. Kule ambako Khilafah itasimamishwa kwanza, iko Mikononi mwa Mwenyezi Mungu Peke Yake, kwani Yeye Pekee hupeana Nasr (ushindi). Bishara njema za Mtume (saw) zinatoa habari (khabar) juu ya jambo la uwezekano. Ama dori yetu ni kufuata njia ya Utume, kusimamisha Uislamu katika kutawala mambo yetu.

Soma zaidi...

Ash-Sham ndio Nyumba ya Khilafah

Tunaweza kusema kwamba kuwasili kwa Khilafah katika Bait ul Maqdis kuna dalili zaidi ya moja. Ya kwanza ni kwamba Bait ul Maqdis ni eneo la kihistoria, kisiasa na kijografia la ulimwengu wa kale. Ni kitovu cha dini zote na kitovu cha umakini wao. Yeyote anayeidhibiti atatawala ulimwengu wa zamani. Hii ina maana kwamba pale Khilafah itakaposimamishwa, basi Waislamu watatawala ulimwengu mzima licha ya Mayahudi na Wakristo kuwa dhidi yao. Pili ni malipo kwa watu wa Ash-Sham kwa yale yaliyowapata na maumivu, kuvunjika, subira na uvumilivu waliyopitia kwa miongo mingi.

Soma zaidi...

Dola ya Kiislamu Inautaka Uislamu Kuwa ndio Msingi wa Sheria na Hukmu Zote, Sio Baadhi ya Sheria Zilizopitishwa na Mahakama Bandia ya Shariah

Hukmu kubwa imepitishwa na Mahakama ya Shirikisho ya Shariah ya Pakistan. Ilitangaza vifungu vichache vya sheria ya Waliobadili Jinsia ya 2018 kama kinyume na Uislamu. Kwa hivyo, vitakoma kutekelezwa, ilhali sheria iliyosalia itabaki kutekelezwa.

Soma zaidi...

Dori ya Kuisimamisha Dola ya Khilafah katika Mzozo wa Sasa wa Kimataifa juu ya Nani Ataitawala Dunia

Mizozo ya kimataifa imekuwepo muda wote wa historia ya mwanadamu na imeendelea kuwa mibaya zaidi katika muda wa sasa. Kila muda ukisonga, dunia hii ya kisasa inashuhudia mizozo ya kutisha zaidi katika historia ya mwanadamu, ikiuwa mamilioni ya watu katika hali ya kikatili kutokana na maendeleo ya silaha za kisasa

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu