Ulaya Yahangaika Siku Chache Tu Bila Mafuta na Gesi ya Waislamu: Vipi Basi Ikiwa Ummah Ungeamka?!
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Waziri wa Fedha wa Ufaransa Roland Lescure alisema kwamba serikali haziwezi kuamua kama zitoe akiba ya ziada ya mafuta ya kimkakati ili kupunguza usumbufu unaosababishwa na vita vya Iran hadi muda unaowezekana wa mzozo huo utakapokuwa wazi. Katika muktadha huo huo, mashambulizi ya awali ya makombora ya Iran kwenye kituo cha gesi cha Ras Laffan nchini Qatar, mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya gesi asilia vilivyoyeyushwa duniani, yalisababisha kupungua kwa kasi kwa akiba ya gesi ya Uingereza. Akiba ya gesi asilia nchini Uingereza ilishuka hadi viwango vya kutosha kukidhi matumizi ya ndani kwa muda usio zidi masaa 48.



