Katika Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Khilafah... Dunia Inajitayarisha Kurudi Kwake
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mtu anaweza kufikiri, huku akiangalia yanayojiri hivi karibuni katika ngazi ya kimataifa na katika ardhi za Kiislamu, kwamba uhalisia unazidi kuwa wa giza tororo kwa Umma wa Kiislamu, na kwamba matumaini ya kuamka kwake na kuregeshwa kwa heshima yake yanafifia au kupungua. Hata hivyo, kutafakari haya yanayojiri kunaonyesha kwamba yanafichua matumaini ambayo yanajajidishwa na kuzidi kuwa makubwa, na mbinu ya kuelekea mwamko siku baada ya siku.



