Ijumaa, 03 Ramadan 1447 | 2026/02/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Pongezi kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Wanaozuru Kurasa zake kwa Mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wa Mwaka 1447 H sawia na 2026 M
(Imetafsiriwa)

Kwa Umma bora uliotolewa kwa ajili ya wanadamu... Umma wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameuheshimu kwa utiifu Wake...

Kwa wabebaji Dawah watukufu ambao biashara wala uuzaji haziwazuii kumkumbuka Mwenyezi Mungu; Mwenye Nguvu, Mwenye Hekima...

Kwa wageni watukufu wanaozuru ukurasa wanaokuja kwenye kheri unayoibeba...

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh,

Sifa zote njema ni kwa Mwenyezi Mungu na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake na maswahaba zake na wale wanaomfuata.

Namuomba Mwenyezi Mungu akubali funga na Qiyaam za Waislamu na Mwenyezi Mungu atusamehe madhambi yetu yote yaliyotangulia, kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kama alivyopokea Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «مَنْ صَامَ رَمَضَانَ، إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا،غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ» “Atakayefunga Ramadhan kwa imani na kutaka malipo yake kwa Mwenyezi Mungu atasamehewa madhambi yake yaliyopita” na katika riwaya nyengine kutoka kwa Abu Hurayrah (ra) amesema kwamba Mtume wa  Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ» “Mwenye kuswali Qiyaam (swala ya hiari ya usiku) katika Ramadhan kwa imani na kutaka malipo yake kwa Mwenyezi Mungu atasamehewa madhambi yake yaliyopita.”

Wapendwa kina kaka na dada waheshimiwa, katika mwezi wa Sha’ban mwaka wa pili baada ya Hijra, Mwenyezi Mungu Mtukufu alifaradhisha kufunga mwezi wa Ramadhan. Ni mwezi ambao Mwenyezi Mungu aliteremsha ndani yake Quran:

[شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ]

“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi.” [Al-Baqara: 185[. Ni mwezi ambao Mwenyezi Mungu aliutukuza Ummah kwa ushindi na fursa za kipekee. Kwa kuwa Vita Vikuu vya Badr vilikuwa tarehe 17 Ramadhan wakati washirikina wa Makka waliposhindwa kabisa... Kisha kulikuwa na vita vyengine muhimu katika mwezi huu uliobarikiwa, kuanzia na ufunguzi wa Makka tarehe 20 Ramadhan katika mwaka wa nane baada ya Hijra hadi Vita vya al-Buwayb (vilivyo karibu na mji wa Kufa kwa sasa) ambayo ilikuwa Yarmouk ya Fursi wakati Waislamu waliposhinda chini ya uongozi wa al-Muthanna tarehe 12 Ramadhan ya mwaka wa 13 H, kisha hadi ufunguzi wa Amuriyah ukiongozwa na Al-Mu’tassim tarehe 17 Ramadhan katika mwaka wa 223 H, na hadi Vita vya Ayn Jaloot wakati Waislamu walipowashinda Matatari mnamo tarehe 25 Ramadhan katika mwaka wa 658 H hadi ushindi mwingine katika mwezi huu uliobarikiwa.

Kwa hivyo, kufunga kuliambatana na Qur'an Tukufu ambako hakuwezi kuathiriwa na batili mbele yake au nyuma yake... Kufunga kuliambatana na ufunguzi na ushindi wa kipekee... Kufunga kuliambatana na jihad... Kufunga kuliambatana na utabikishaji wa Sheria za Mwenyezi Mungu... Na mtu yeyote mwenye maono na ufahamu wazi anatambua kwamba Sheria za Mwenyezi Mungu haziwezi kutenganishwa, iwe ni matendo ya ibada au jihad au miamala au akhlaki na mwenendo, au uhalifu na Hudud (adhabu)... Kwani haya yote yanatoka katika sehemu moja, na yeyote anayetafakari aya za Qur'an Tukufu na maandiko ya Hadith tukufu anaona kwamba hili limefafanuliwa waziwazi. Hivyo, Uislamu ni kitu kisichogawanyika, na wito wake ni ule unaopaswa kutekelezwa ndani ya dola, maisha na jamii. Kwa hivyo yeyote anayetenganisha kati ya aya za Mwenyezi Mungu, na kulingania kutenganishwa kwa Dini na maisha, au kutenganishwa kwa Dini na siasa, amefanya dhambi kubwa na uhalifu mkubwa unaompeleka mtu kwenye aibu katika ulimwengu huu na adhabu kali Akhera.

Enyi Waislamu, nawakumbusha haya yote katika siku hizi ambapo uvamizi wa kikatili wa Mayahudi dhidi ya Ukingo wa Magharibi pamoja na Gaza unaendelea, kisha uvamizi wa Mayahudi ukaenea hadi Lebanon na Syria… ambapo waliranda wakiwa huru katika nchi za Kiislamu bila kukutana na upinzani wowote wa kweli. Badala ya watawala kuhamasisha majeshi ya Waislamu kupigana na umbile la Kiyahudi, kuwafukuza wale walio nyuma yake na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa... badala yake, tunawaona watawala hawa wakisaini makubaliano baada ya makubaliano nalo, na hata mtawala dhalimu Trump anawakusanya pamoja ili kuwadhalilisha, bila aibu yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, au waumini!

Hata hivyo, Enyi Waislamu, vita dhidi ya Mayahudi, mauaji yao, na kuondolewa kwa umbile lao lazima yawe chini ya uongozi wa Khalifa Rashid (Khalifa muongofu) baada ya utawala huu dhalimu na watawala vibaraka. Bishara njema za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) hazitacheleweshwa, Mwenyezi Mungu akipenda, katika kutimiza yale aliyoyapokea Ahmad kutoka kwa Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) isemayo: «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ» “Kisha utakuweko utawala wa kidhalimu, na utakuwepo kama Mwenyezi Mungu atakavyo uwe, kisha atauondoa anapotaka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza.” Na pia katika uthibitisho wa hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, ambayo imepokewa na Muslim «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...» “Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na kwa yakini mtawaua...”

Kwa kumalizia, kama tunavyopaswa kuwa na bidii katika funga yetu ili Mwenyezi Mungu afurahi nasi na atusamehe dhambi zetu za awali, vivyo hivyo tunapaswa pia kuwa na bidii kufanya kazi kwa ajili ya kuregeshwa kwa maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ili tuwe miongoni mwa washindi katika maisha haya kwa utekelezaji wa Sheria za Mwenyezi Mungu, zilizofunikwa na bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Rayat Al-Uqab, bendera ya La Illaha Illah Allah Muhammad Rasoul Allah na vivyo hivyo tuwe washindi kesho Akhera, Mwenyezi Mungu akipenda, wale wanaotafuta kimbilio katika kivuli chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli ila kivuli chake, ili tuweze kupata ushindi katika maisha yote mawili. Hakika huo ndio ushindi mkubwa.

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh.

1 Ramadhan 1447 H
Sawia na 18/02/2026 M

Ndugu Yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu