Hotuba ya Mwanachuoni na Amiri wa Hizb ut Tahrir Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah (Mwenyezi Mungu amlinde) Katika Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Khilafah
- Imepeperushwa katika Hotuba
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika siku hizi kama hizi, miaka 105 iliyopita, mwishoni mwa Rajab 1342 H, sambamba na mapema Machi 1924 M, wakoloni makafiri, wakiongozwa na Uingereza wakati huo, kwa ushirikiano na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, waliweza kuivunja Khilafah. Mhalifu wa zama hizo, Mustafa Kemal, alitangaza ukafiri wa wazi kwa kuifuta Khilafah, kumzingira Khalifa jijini Istanbul, na kumfukuza alfajiri siku hiyo hiyo. Hivyo, tetemeko baya la ardhi lilizikumba ardhi za Waislamu kwa kuvunjwa Khilafah, chimbuko la izza yao na radhi ya Mola wao Mlezi.



