Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 2 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: 1447 H / 080 |
| M. Jumanne, 19 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hali Imefikia Hatua Ambapo Watawala wa Waislamu Wanacheza Kamari na Hatari ya Nyuklia Katikati ya Ardhi za Waislamu!
(Imetafsiriwa)
Afisi ya Habari ya Abu Dhabi iliripoti kwamba timu maalum za kukabiliana na dharura mnamo Jumapili zilidhibiti moto uliozuka katika jenereta ya umeme iliyoko nje ya eneo la ndani la Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Barakah katika eneo la Al Dhafra, kufuatia shambulizi la droni kwenye eneo hilo, bila majeraha yoyote au uvujaji wowote wa mionzi uliorekodiwa. Wizara ya Ulinzi ya Imarati ilieleza kwamba uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha mashambulizi hayo, ikibainisha kuwa maendeleo yoyote yatatangazwa mara tu uchunguzi utakapokamilika.
Kwa kweli, kinachotokea ni uovu mkubwa: kwamba ardhi za Waislamu zimekuwa uwanja ulio wazi na ukumbi wa visasi na kufikia malengo ya kisiasa, bila kujali hali ambayo ardhi za Waislamu zimeharibika, wala hatima ya Waislamu na watu wa eneo hilo hadi kufikia hatua ya kwamba hata kituo cha nyuklia kinalengwa, wala matokeo yote ambayo yanaweza kuwa mabaya kwa eneo hilo na watu wake!
Iwe Iran, Amerika, au umbile la Kiyahudi ndizo zilizo nyuma ya shambulizi hilo, matokeo yake ni kwamba hii ni hali ambayo haiwezi kuvumiliwa kimya kimya. Watawala wa Waislamu pande zote mbili za mgogoro wa sasa ndio walioiwezesha Amerika kuvamia ardhi za Waislamu na kuzipenya. Wao ndio waliofungua ardhi kwa ajili ya kuwekwa idadi ya makumi ya kambi za kijeshi. Wao ndio waliofanya amani na kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi na kuanzisha miradi ya pamoja nalo, na hivyo kuliingiza katika ardhi za Waislamu. Hivyo, baada ya haya yote, imekuwa kawaida kwa ardhi zetu kuwa ukumbi na uwanja kwa wahalifu hawa kutekeleza mipango na miradi yoyote wanayotaka ili kuimarisha udhibiti wao juu yazo.
Watawala wa Waislamu walitembea pamoja na Amerika katika uvamizi wake wa Iraq na Afghanistan na katika kutekeleza miradi yake huko Ash-Sham na Yemen hadi walipoiwezesha katika ardhi za Waislamu. Wanaendelea kuipa Amerika na umbile la Kiyahudi usaidizi wote wa kifedha, vifaa, kijeshi, na kisiasa wanaohitaji ili kufikia malengo yao ya kikoloni. Mwathiriwa katika haya yote ni ardhi za Waislamu, maisha ya Waislamu, na rasilimali zao.
Hivi Ummah utakaa kimya hadi lini kuhusu uongozi wa wasaliti hawa juu yake? Je, wakati haujafika wa kuwaondoa kifuani mwake na kumteua Khalifa mmoja atakayekusanya sehemu zake zilizotawanyika, kuuunganisha, na kukata mkono wa ukoloni kutoka katika ardhi zetu, ili uweze tena kuwa Umma wenye heshima unaoleta izza, badala ya Umma dhaifu na ukumbi wa matukio? Hakika, Wallahi, wakati umewadia.
Mhandisi Salah Eddine Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizbut-tahrir.info |