Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 5 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H 1447 / 082 |
| M. Ijumaa, 22 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Msikose Fursa ya Kuunda Mfumo Mpya wa Kimataifa, Enyi Waislamu — Nyinyi Ndio Watu Wake na Mnaliweza hilo Kupitia Itikadi Yenu Tukufu
(Imetafsiriwa)
Hivi majuzi, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitembelea China, na mwishoni mwa ziara hiyo taarifa ya pamoja ya zaidi ya nukta arubaini ilitolewa. Ndani yake, nchi hizo mbili zilitangaza mikataba na makubaliano kadhaa. Hata hivyo, kinachoonekana katika taarifa hiyo ni wito wa nchi zote mbili wa mpangilio mpya wa ulimwengu wa nchi nyingi. Pia inaeleweka kwamba ziara ya Putin nchini China ilikuja baada ya ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump nchini China, na baada ya ziara ya Putin kukamilika ilitangazwa kwamba rais wa China anakusudia kutembelea Korea Kaskazini.
Bila kujali malengo na ujumbe wa ziara hizi, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafafanua nukta zifuatazo:
Kwanza: Tangu Vita vya Pili vya Dunia, dunia imeishi chini ya dhulma, ukandamizaji, na ukoloni unaotokana na utawala wa Marekani na uongozi wake wa kambi ya kibepari ya Magharibi dhidi ya kambi ya kikomunisti ya Mashariki, ikifuatiwa na enzi ya Vita Baridi. Hii iliendelea hadi kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti mwanzoni mwa miaka ya tisiini, baada ya hapo Marekani ikawa na nguvu ya kipekee katika masuala ya kimataifa. Ilianzisha utaratibu wa ulimwengu wa kikoloni kulingana na zana kadhaa, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa na matawi yake, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia, watawala vibaraka, na kaulimbiu za haki za binadamu, haki za watoto, haki za wanawake, na zengine.
Pili: Waislamu wamekuwa wahanga wakubwa wa utaratibu huu wa kimataifa ulioanzishwa na Amerika ili kuimarisha utawala wake wa kimataifa na kukoloni na kupora kile inachoweza. Ilivamia ardhi za Waislamu kwa visingizio vya kirongo, na kuwaua mamilioni—hasa Afghanistan na Iraq—na kuwaweka watawala vibaraka ndani yake. Pia iliwadumisha watawala vibaraka katika ardhi za Waislamu kuendelea kupora rasilimali zao na kuzuia umoja wao na kuanzishwa kwa Khilafah. Hivi majuzi, pamoja na umbile lake la uwakilishi Israel, ilianzisha vita dhidi ya Iran.
Tatu: Ziara ya Putin nchini China iliambatana na mazoezi ya kijeshi ya Urusi yaliyodumu kwa siku tatu, kuonyesha nguvu za nyuklia, chini ya dhana kwamba nguvu za kijeshi pekee zinaweza kuunda uwepo wa kimataifa na kubadilisha siasa za kimataifa. Hii inaakisi usemi wa majivuno wa Trump akidai ana jeshi lenye nguvu zaidi duniani. Wote wanafuata fikra ile ile kama watu wa 'Aad waliposema:
[مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً]
“Nani aliye kuwa na nguvu kushinda sisi?” [Fussilat:15]. Jibu la wahyi likaja:
[أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ الَّذِي خَلَقَهُمْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً]
“Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba ni Mwenye nguvu kushinda wao?” [Fussilat:15].
Nne: Kauli ya Urusi na China ilitegemea katika nukta zake nyingi kuhusu Umoja wa Mataifa, ambao ulianzishwa na Amerika, na mashirika mengine ya kimataifa kama vile Shirika la Shanghai, BRICS, Muunganio wa Uchumi wa Ulaya na Asia, na mengineyo—kufuata njia ile ile ya Magharibi ya kambi na miungano ambayo imesababisha mateso kwa ulimwengu tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Tano: Haipaswi kuwa na sheria ya kimataifa kwa maana ya mfumo wa kisheria unaozifunga dola, wala haipaswi kuwa na dola ya kimataifa inayodhibiti mambo ya dunia. Kila dola ina mamlaka na uhuru wake, na hakuna mtu mwenye mamlaka juu yake. Badala yake, kilichopo ni mikataba ya kimataifa iliyokubaliwa na dola kudhibiti mambo ya pamoja—sawa na Hilf al-Fudul, mkataba ulioshuhudiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kabla ya utume, ambapo makabila yalikubali kuwasaidia wanaokandamizwa. Baada ya utume, yeye (saw) alisema: «لَقَدْ شَهِدْتُ فِي دَارِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ جُدْعَانَ حِلْفًا، مَا أُحِبُّ أَنَّ لِي بِهِ حُمْرَ النَّعَمِ، وَلَوْ أُدْعَى بِهِ فِي الْإِسْلَامِ لَأَجَبْتُ» “Nilishuhudia katika nyumba ya Abdullah ibn Jud’an mapatano ya kwamba sitaki kuwa na ngamia wekundu badala yake, na kama ningeitwa katika Uislamu, ningeitikia.” (Imesimuliwa na Al-Bayhaqi)
Sita: Tunawakumbusha Waislamu kuhusu kufeli kwa mfumo wa kibepari ambao Amerika na Ulaya zimejikita, na mateso ambayo yamesababisha dunia kwa ujumla na hasa Waislamu. Pia tunabainisha kwamba dola kubwa zinazoinuka—Urusi na China—hazina mfumo wowote tofauti; pia zinafanya kazi ndani ya mfumo wa kibepari. Kwa kukosekana Khilafah na chini ya utawala wa kibepari, mahusiano ya kimataifa yameegemea maslahi, unyonyaji, migogoro kuhusu rasilimali, na vita ambavyo vimechukua mamilioni ya maisha na kumwaga mito ya damu.
Hatimaye, hakuna anayestahili zaidi yenu, Enyi Waislamu, kuanzisha mfumo wa kimataifa wa haki unaoegemea uadilifu, nusra kwa wanaokandamizwa, na afueni kwa walio na dhiki. Nyinyi pekee mna mfumo sahihi ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu—mfumo uliotawala dunia kwa zaidi ya karne kumi na mbili, ambapo wanadamu walishuhudia uadilifu wa Uislamu bila kujali dini, rangi, au asili. Ulimwengu ulishuhudia hili—marafiki na maadui vile vile.
Msiseme kwamba nyinyi ni madhaifu na mmegawanyika; mna uwezo wa kuchukua hatua kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo Hizb ut Tahrir inakulinganieni kuisimamisha. Ndani yake imo heshima yenu katika dunia hii na wokovu katika Akhera, na ndani yake umo uokozi wa wanadamu kutokana na udhalimu wa ubepari. Kwa hivyo fanyeni haraka kufanya kazi na Hizb ut Tahrir na kuiunga mkono.
[وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]
“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Al-Hajj:40]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizbut-tahrir.info |