Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Maoni ya Habari 09/04/2025 M
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Maoni ya habari yaliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan.
Maoni ya habari yaliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan.
Bila jeshi hata moja la Waislamu kumzuia, Trump alitimiza ahadi yake ya kufanya maangamizi makubwa Gaza. Kamera zimenasa picha za sehemu za miili ya waumini zikipaa angani, juu ya majengo marefu, kutokana na kukithiri kwa mashambulizi ya makombora. Madaktari wa uokoaji wanafunikwa macho na kupigwa risasi. Watoto, wanawake, wazee na waliojeruhiwa wanauawa shahidi kwa kulipuliwa mahema yao. Sera ya njaa ya Amerika, iliyotekelezwa na wafuasi wake, umbile la Kiyahudi, imeongeza mateso hadi kiwango cha baa la njaa. Sasa imedhihirika kwa kila mtu kwamba Firauni wa Washington anafanya maangamizi makubwa kwa Gaza, kwa usaidizi kamili wa kijeshi na uongozi wa kisiasa wa Waislamu na Mayahudi.
Mnamo tarehe 3 Aprili 2025, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ilitangaza kwamba “inalaani vikali uvamizi unaoendelea na unaozidi kuongezeka wa Israel.” Shirika hilo linajisifu kama “sauti inayounganisha ulimwengu wa Kiislamu.” Lakini watu wa Gaza hawahitaji “sauti,” bali vitendo kutoka kwa majeshi ya Waislamu.
Sisi ni Umma wa watu bilioni mbili, na Pato la Taifa ni $8.7 trilioni na usawa wa nguvu ya ununuzi ya $26.4 trilioni. Tuna akiba kubwa zaidi ya nishati na madini ulimwenguni, na idadi kubwa vijana changamfu. Sehemu inayokosekana ya mlingano huo ni uongozi mnyoofu wa kisiasa, Khilafah Rashida. Swali pekee lililobaki ni: Je, tuko tayari kupambana na kujitahidi kusimamisha dini ya Mwenyezi Mungu ndani ya dola ya Khilafah?
Mnamo tarehe 31 Machi 2025, jeshi la Kiyahudi lilitoa maagizo makubwa ya kuwahamisha watu wa Rafah na maeneo ya karibu. Enyi majeshi ya Waislamu! Adui yenu ametangaza kukoleza vita, na bado hamujajiunga na vita, baada ya miezi kumi na nne! Haaman, jemadari wa Firauni dhalimu wa Misri, sasa yuko Motoni, pamoja na jeshi lake. Kuwatii madhalimu si udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu ﷻ. Wapunguzieni majeshi mizigo ya Mafirauni wa leo. Mteueni Khalifa Rashid na musonge kuinusuru Gaza. Au munasubiri kuungana na Haaman na jeshi lake? Au mnangoja kubadilishwa na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu pekee?
Maoni ya habari yaliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Pongezi kwa Mnasaba wa Ujio wa Idd ul-Fitr 1446 H
Kufuatia mashambulizi ya kikatili ya Gaza na umbile la Kiyahudi, umbile hilo lilipanua mashambulizi yake ya ardhini huko Gaza mnamo 20 Machi 2025. Wakati huo huo, viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Waislamu wanashughulika kumfurahisha Farauni wa Washington, Trump, na majeshi yetu yanatumiwa katika vita vya uasi. Tunaweza kuuliza majeshi ya Waislamu: Je, si ndugu zenu Waislamu ndio walioifanya Marekani ionje kushindwa nchini Iraq na Afghanistan?
Televisheni ya serikali ya Pakistan ilisema mnamo 19 Machi 2025: “Pakistan inalaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel.” Hivi ndivyo watawala wa Pakistan walivyolaani hujuma ya Mayahudi na jinai zake zinazoendelea dhidi ya Ukanda wa Gaza! Bila kusonga askari au kuinua silaha!
Maneno yanashindwa kuelezea uhalifu huu wa kutisha katika mwezi huu mtukufu. Mayahudi wa Netanyahu na Marekani ya Trump wanawaonea watu wasio na hatia huku wakiwa wamelala, wakitumia ndege 100, zikiwemo ndege za kivita za Marekani, kulenga mahema yaliyojaa raia, kwa kisingizio kwamba wapiganaji wachache wa upinzani wapo. Waliwafuatiulia huku kukiwa na udanganyifu waliouita "usitisha mapigano"!