Alhamisi, 17 Sha'aban 1447 | 2026/02/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Jibu la Swali: Ni Yapi Yaliyo Nyuma ya Ongezeko la Mgogoro wa Yemen

Baada ya vikosi vya Baraza la Mpito la Kusini (STC) nchini Yemen, vikiongozwa na Aidarus al-Zubaidi, mjumbe wa Baraza la Rais, kupeleka vikosi vyao huko Hadramawt na al-Mahrah, hali ikawa ngumu sana. Rais wa STC Rashad al-Alimi alisitisha makubaliano ya pamoja ya ulinzi na Imarati na kudai kwamba iondoe vikosi vyake kutoka Yemen ndani ya masaa 24. Saudi Arabia ilimuunga mkono mara moja na kushambulia silaha za Imarati katika Bandari ya Mukalla. Kisha Saudi Arabia ilidai kwamba Imarati itii matakwa ya Rashad al-Alimi na kuondoa vikosi vyake kutoka Yemen. Imarati baadaye iliondoka, na hatimaye, al-Zubaidi alikimbilia Imarati. Kwa hivyo, ni nini kilicho nyuma ya kuongezeka huku kwa mgogoro wa Yemen? Je, Uingereza inapoteza washirika wake nchini Yemen? Na je, mzozo huu una vipimo vya kimataifa?

Soma zaidi...

Katika Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Khilafah... Dunia Inajitayarisha Kurudi Kwake

Mtu anaweza kufikiri, huku akiangalia yanayojiri hivi karibuni katika ngazi ya kimataifa na katika ardhi za Kiislamu, kwamba uhalisia unazidi kuwa wa giza tororo kwa Umma wa Kiislamu, na kwamba matumaini ya kuamka kwake na kuregeshwa kwa heshima yake yanafifia au kupungua. Hata hivyo, kutafakari haya yanayojiri kunaonyesha kwamba yanafichua matumaini ambayo yanajajidishwa na kuzidi kuwa makubwa, na mbinu ya kuelekea mwamko siku baada ya siku.

Soma zaidi...

Hotuba ya Mwanachuoni na Amiri wa Hizb ut Tahrir Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah (Mwenyezi Mungu amlinde) Katika Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Khilafah

Katika siku hizi kama hizi, miaka 105 iliyopita, mwishoni mwa Rajab 1342 H, sambamba na mapema Machi 1924 M, wakoloni makafiri, wakiongozwa na Uingereza wakati huo, kwa ushirikiano na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, waliweza kuivunja Khilafah. Mhalifu wa zama hizo, Mustafa Kemal, alitangaza ukafiri wa wazi kwa kuifuta Khilafah, kumzingira Khalifa jijini Istanbul, na kumfukuza alfajiri siku hiyo hiyo. Hivyo, tetemeko baya la ardhi lilizikumba ardhi za Waislamu kwa kuvunjwa Khilafah, chimbuko la izza yao na radhi ya Mola wao Mlezi.

Soma zaidi...

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Angazo la Amali za Kimataifa za Hizb ut Tahrir katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa Khilafah 1447 H – 2026 M

Katika mwezi mtukufu wa Rajab wa mwaka huu, 1447 H (2026 M), tunakumbuka kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, vibaraka wa wakoloni makafiri. Dola hii ilianzishwa na Bwana wa Mitume, Muhammad (saw), na Maswahaba zake Watukufu (ra). Mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) uliondolewa mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na 3 Machi 1924 M, mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal.

Soma zaidi...

Kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 105, Tunaufufua Wito kwa Majeshi Yote ya Ummah Kuhamasisha Nguvu Zao Ili Kusimamisha Khilafah Rashida

Mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na tarehe 3 Machi, 1924 M, amri ovu ilitolewa na lile lililoitwa Bunge Kuu la Kitaifa, ikielezea kufutwa rasmi kwa Khilafah. Kwa kuvunjwa kwa Khilafah, hukmu za Sharia ziliondolewa, kiapo cha utiifu (Bay’ah) kilisitishwa, na ardhi za Waislamu zilichanwa vipande vipande kwa misingi ya kitaifa na kikabila kuwa vijidola tete, tegemezi, na dhaifu. Vibaraka wa kulipwa waliteuliwa kuzitawala. Fikra ya umoja ilipigwa pigo kubwa. Kwa kuangamia kwake, Bayt al-Maqdis na Ardhi Iliyobarikiwa zilianguka, na umbile lenye saratani la Kiyahudi lilipandwa katikati ya ardhi za Waislamu.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu