Swahaba Mtukufu Mus’ab ibn Umair, Mwenyezi Mungu (swt) Amuwie Radhi
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika kundi la majina yenye kung'aa ya maswahaba watukufu, jina la Mus’ab bin Umair (ra) linajitokeza kama ishara ya muhanga na uthabiti. Mus’ab alikuwa mshika mwenge wa Da’wah katika hatua zake zote, kwani alikuwa ni kijana miongoni mwa vijana bora wa Makka, aliyejulikana kwa uzuri wake, harufu ya kupendeza, na maisha ya anasa, kiasi kwamba Maswahaba, Mwenyezi Mungu (swt) awawie radhi wote, wakasema juu yake, ما رأينا بمكة أحدا انعم عيشا من مصعب بن عمير “Hatujamuona mtu yeyote mjini Makka ambaye aliishi kwa neema kuliko Mus’ab bin Umair.”



