Ufisadi wa Mfumo Huzalisha Ufisadi katika Masuluhisho Sera ya Ufukarishaji: Zawadi ya Idd al-Adha kutoka kwa Watawala kwa Watu wa Yemen
- Imepeperushwa katika Yemen
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Serikali ya Shaea Al-Zandani mnamo Jumanne, 19/05/2026, ilianzisha hatua mpya ya kiuchumi ambapo ilipandisha bei ya dolari ya ushuru wa forodha kwa zaidi ya 100%, kutoka riyali 750 hadi riyali 1,550, na kuongeza bei ya chombo cha dizeli cha lita 20 kwa 24.5%, ikiruka kutoka riyali 29,500 hadi 36,000. Kisha ilijaribu kuwaziba macho watu wa Yemen kwa kuidhinisha posho ya gharama ya maisha ya 20% kwa wafanyikazi wa sekta ya umma, pamoja na kuwapa nyongeza yao ya kila mwaka inayostahili kwa miaka ya 2021-2024, na kufanya marekebisho ya viwango vya kazi ambayo yalikuwa yamesimamishwa kwa zaidi ya miaka 13.



