Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
| H. 3 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H 1447 / 28 |
| M. Jumatano, 20 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
ACSA na GSOMIA: Watu Wenye Ufahamu na Wanasiasa Wenye Ikhlasi Wanapaswa Kujitokeza Kuilinda Nchi Isije Kuwa Nchi ya Kitumwa
(Imetafsiriwa)
Inatisha sana kwa watu wa Bangladesh, wakati vyanzo mbalimbali vinathibitisha kwamba Marekani na Bangladesh zinaendelea na mfululizo wa mikataba ya ulinzi na biashara chini ya ‘Mkataba wa Biashara wa Pamoja (ART)’ wa kikoloni. Kampeni ya Marekani ya GSOMIA ilihama kutoka fahamu dhahania hadi ramani halisi mnamo Machi 2022, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wa wakati huo Victoria Nuland alipowasilisha rasimu ya Mkataba Mkuu wa Usalama wa Taarifa za Kijeshi (GSOMIA) ndani ya mfumo wa Mkakati wa Marekani wa Indo-Pacifiki (IPS) ulitarajiwa mnamo 2017 na kuandikwa mnamo 2019. Ingawa ziara ya Nuland ilikuwa alama muhimu kwa GSOMIA, Mkataba wa Upataji na Huduma Mtambuka (ACSA) uliinuliwa rasmi mnamo Aprili 2019 na kuitekelezwa wakati wa Mazungumzo ya 7 ya Usalama jijini Dhaka. Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh imekuwa ikiwaonya watu na wanasiasa kwamba Bangladesh iko karibu kusaini mikataba miwili mikubwa ya kijeshi ya Marekani - GSOMIA na ACSA - ambayo hatari zake halisi sasa zinajitokeza huku ushawishi wa Marekani wa kuharakisha mikataba hii inayoharibu uhuru ikiingia katika hatua yake ya mwisho. Chini ya mfumo huu, GSOMIA inaweza kuilazimisha Bangladesh kuoanisha akili na malengo ya kikanda ya Marekani, na kuiingiza katika migogoro isiyohitajika, huku ACSA ikiweza kuwezesha “kambi hafifu” kama ilivyo katika Bazar ya Cox - aina ya ushawishi wa ukoloni mamboleo unaohujumu kutoegemea upande wowote wa kimkakati.
Tangu 2009, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh imekuwa chama pekee cha kisiasa kinachopiga kelele dhidi ya ukoloni hafifu wa Marekani, ikionya Ummah kwamba ni aina hiyo hiyo ya makubaliano ya kijeshi ya ACSA yaliyoshinikizwa dhidi ya Sri Lanka baada ya 9/11 kudhibiti maji ya kimkakati sasa yanaleta tishio lile lile la ubwana kwa Bangladesh. Mnamo Machi 2026, kufuatia ziara ya Waziri Msaidizi wa Marekani Paul Kapur na ushawishi mkali wa Marekani kwa GSOMIA na ACSA, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh iliandaa maandamano baada ya swala za Ijumaa jijini Dhaka na Chittagong, ikiangazia ombi la Rais Trump mwenyewe kwa Waziri Mkuu wa Bangladesh kuchukua “hatua kali” ili kukamilisha mikataba hii inayo momomnyoa ubwana wa kujitawala.
Je, watawala wa nchi wanaamini kwamba uhai wao unategemea Washington? Ilhali Washington haiwezi kamwe kumlinda mtawala yeyote kutokana na hasira za watu. Badala yake Marekani huosha mikono kwa kushirikiana na watu katika kuanguko kwa utawala unaopinga watu, kisha kutafuta njia badali. RasulAllah (saw) alionya kuhusu “Ruwaibidha” - waovu na wapumbavu wanaotumikia utawala wa Magharibi na kusaliti imani ya umma. Huku watawala wanaweka rehani mustakabali wa Ummah kwa usalama wa muda, wakijifanya kama vibaraka, sio viongozi. Je, tuna matumaini yoyote kutoka kwa vyama vya kisiasa vilivyopo ambavyo haviko tayari Kusema Hapana Kabisa kwa Washington na Kulinda Uhuru wa Watu?
Na, wako wapi ‘Waturuki Vijana’ wa Mapinduzi ya Julai? Wanabaki kimya kuhusu ukoloni mamboleo wa Marekani na mikataba hii ya kupinga uhuru, badala yake wakitaka kubaki katika maelewano mazuri na Marekani kama vyama vyengine vyote. Je, pia nao wanakuwa marafiki wa Marekani ya kikoloni? Kimya hiki ni usaliti. Mikataba hii ya biashara na kijeshi ni kipimo kwa vyama hivi vinavyodai kuwawakilisha watu - historia inatoa onyo wazi. Wanatoa hoja ya kuialika ‘Marekani’ kujilinda kutokana na ‘India’. Je, huku si kumualika ‘mbwa mwitu’ kujilinda kutokana na ‘dubu’?
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inamualika kila raia mwenye ufahamu, wanasiasa wenye ikhlasi, na Maafisa Wakweli katika Jeshi letu kuacha kupoteza nguvu kwa vyama ambavyo kimya chao kuhusu mikataba hii ya ulinzi kinathibitisha kuwa hawana nia ya kulinda uhuru wenu. Msidanganyike na kaulimbiu zao. Wanataka kuwauza kwa utawala wao. Ni siasa za kurudisha Khilafah kwa njia ya Utume pekee ndizo zinazoweza kuchukuliwa kuwa za kweli na za ikhlasi. Ni Khilafah pekee inayoweza kuwa na ujasiri na uwezo wa kusimama dhidi ya vitisho vya kijeshi vya Marekani, shinikizo la kiuchumi, na kuzingirwa kimkakati. Khilafah haitaomba mikataba ya kibiashara kwa gharama ya ardhi yake. Haitafanya biashara bandari zake kwa ushuru wa nguo. Itamsujudia Mwenyezi Mungu (swt) pekee.
[وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً]
“…wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surah An-Nisa:141].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |



