Jumamosi, 13 Dhu al-Hijjah 1447 | 2026/05/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Msikose Fursa ya Kuunda Mfumo Mpya wa Kimataifa, Enyi Waislamu — Nyinyi Ndio Watu Wake na Mnaliweza hilo Kupitia Itikadi Yenu Tukufu

Hivi majuzi, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitembelea China, na mwishoni mwa ziara hiyo taarifa ya pamoja ya zaidi ya nukta arubaini ilitolewa. Ndani yake, nchi hizo mbili zilitangaza mikataba na makubaliano kadhaa. Hata hivyo, kinachoonekana katika taarifa hiyo ni wito wa nchi zote mbili wa mpangilio mpya wa ulimwengu wa nchi nyingi. Pia inaeleweka kwamba ziara ya Putin nchini China ilikuja baada ya ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump nchini China, na baada ya ziara ya Putin kukamilika ilitangazwa kwamba rais wa China anakusudia kutembelea Korea Kaskazini.

Soma zaidi...

Ufisadi wa Mfumo Huzalisha Ufisadi katika Masuluhisho Sera ya Ufukarishaji: Zawadi ya Idd al-Adha kutoka kwa Watawala kwa Watu wa Yemen

Serikali ya Shaea Al-Zandani mnamo Jumanne, 19/05/2026, ilianzisha hatua mpya ya kiuchumi ambapo ilipandisha bei ya dolari ya ushuru wa forodha kwa zaidi ya 100%, kutoka riyali 750 hadi riyali 1,550, na kuongeza bei ya chombo cha dizeli cha lita 20 kwa 24.5%, ikiruka kutoka riyali 29,500 hadi 36,000. Kisha ilijaribu kuwaziba macho watu wa Yemen kwa kuidhinisha posho ya gharama ya maisha ya 20% kwa wafanyikazi wa sekta ya umma, pamoja na kuwapa nyongeza yao ya kila mwaka inayostahili kwa miaka ya 2021-2024, na kufanya marekebisho ya viwango vya kazi ambayo yalikuwa yamesimamishwa kwa zaidi ya miaka 13.

Soma zaidi...

Salamu za Idd Idd ni Wakati Ambapo Furaha na Huzuni Zinaunganishwa!

Siku hizi Idd al-Adha inafika, ambapo furaha na huzuni zimechanganyika. Furaha katika mwitikio wa waumini kwa wito wa Mwenyezi Mungu wa Hijja, wakiitikia wito wake katika mkusanyiko unaowaunganisha kutoka pembe zote za dunia, pamoja na makabila na rangi zao mbalimbali, kwa kutii amri ya Mwenyezi Mungu na kupata radhi Zake. Na huzuni kubwa inawakumba nyoyo zao kwa masaibu yao tangu kupoteza nguvu yao na kuvunjwa kwa dola yao mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Ni Idd ya aina gani huku Gaza ikiendelea kutokwa na damu?! Idd ya aina gani huku kambi na meli za kivita za maadui wa Umma zikiwa katikati ya ardhi zake?! Idd ya aina gani huku wanawake huru wa Waislamu wakidhalilishwa huko Palestina, Turkestan Mashariki, Myanmar, na India?!

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Kutafuta Nusra kutoka kwa Watawala wa Waislamu wa Zama Hizi

Assalamu alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu. Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba ujumbe wangu utakufikia ukiwa na afya njema zaidi. Swali langu, ewe Sheikh muheshimiwa, ni hili:  Hii ni Hadith sahih iliyopokewa na Masheikh wawili (Bukhari na Muslim) kutoka kwa Mtume (saw) yenye lafudhi: وَإِنَّ اللَّهَ لَيُؤَيِّدُ هَذَا الدِّينَ بِالرَّجُلِ الْفَاجِرِ  “Hakika, Mwenyezi Mungu huenda akaipa nguvu dini hii hata kupitia mtu muovu.”

Soma zaidi...

Salamu za Idd al-Adha Iliyobarikiwa

Tunafurahi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, kuupongeza Ummah mzima wa Kiislamu, na haswa watu wa Sudan, kwa kuwasili kwa Idd al-Adha iliyobarikiwa, tukimwomba Mwenyezi Mungu, Mtukufu, Mwenye Nguvu Zote, kuirudisha tena huku Ummah ukiwa umeungana chini ya umbo lake linalounganisha; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na umeachwa huru kutokana na minyororo ya utumwa kwa wakoloni makafiri wa Magharibi, ukiwa umebeba bendera ya mabadiliko, ili wanadamu waweze kujitolea katika ibada kwa Mola Mlezi wa walimwengu.

Soma zaidi...

Pongezi kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Waislamu kwa Jumla na Mashababu (Wanachama wa Hizb) Hasa kwa Mnasaba wa Sikukuu ya Idd al-Adha 1447 H Sawia na 2026 M

Wapendwa ndugu na dada: Idd hii inakuja huku uvamizi wa Mayahudi, unaoungwa mkono na Amerika na silaha zake, ukiendelea dhidi ya Gaza (Hashim) na Palestina yote. Watawala katika nchi za Kiislamu wanaangalia kinachoendelea, wakiwahesabu mashahidi (shuhadaa) na kuwaita wafu! Na bora zaidi kati yao ni wale wanaopatanisha kana kwamba hawaegemei upande wowote, lakini wako karibu zaidi na Mayahudi!

Soma zaidi...

Watawala wa Pakistan Wanatoa Kile Ambacho Marekani Imekuwa Ikikiota Siku Zote na Kuiondoa Katika Hatari Yake

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza mnamo Jumamosi, Mei 23, 2026, kwamba makubaliano na Iran yalikuwa karibu kukamilika, akisema, “Makubaliano yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa, yanakaribia kukamilika.” Aliongeza kwamba alikuwa na “wito mzuri sana” na viongozi na maafisa nchini Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Pakistan, Uturuki, Misri, Jordan, na Bahrain kuhusu Iran. Hii ilikuja saa chache baada ya afisa mmoja wa Iran kufichua kwa Al Jazeera kwamba mkataba wa maelewano ulikuwa umefikiwa na mpatanishi wa Pakistan, lakini kwamba Tehran ilikuwa ikisubiri majibu ya Marekani. Afisa huyo aliashiria kwamba Mkuu wa Jeshi la Pakistan Asim Munir alipangwa kutangaza mkataba huo wa maelewano jijini Tehran, lakini alikuwa ameondoka ili kufanya uratibu pamoja na Washington

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu