Misri Imenaswa Kati ya Kiu na Mafuriko! Gharama ya Miongo Kadhaa ya Uzembe na Mapuuza
- Imepeperushwa katika Misri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mgogoro wa mafuriko ambayo yalisomba baadhi ya vijiji vya Misri, na kuzamisha nyumba za makumi ya familia, ni sehemu moja tu ya mgogoro mkubwa na hatari zaidi. Mgogoro huu ni uzembe wa serikali juu wa haki za maji za Misri na kupuuza kwake kwa muda mrefu masuala ya wananchi na usimamizi wa rasilimali za nchi kwa ajili ya kulinda usalama wake na maslahi ya wananchi wake. Mgogoro huu haukutokea ghafla. Badala yake, ni matokeo ya mrundikano mtawalia wa sera zilizofeli ambazo zimekausha serikali zana zake za ulinzi wa maji na kufungua mlango kwa Ethiopia kudhibiti njia ya uhai wa Misri na Sudan kupitia Bwawa Kuu la An-Nahdha la Ethiopia.



